Malaria – maono na uzoefu wa anamed

Translated by Frank Jacob

Utangulizi
Katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara malaria inaua kati ya watu milioni moja hadi mbili kila mwaka, haswa watoto. Utafiti wa karibuni (Machi 2005) umeonyesha kuwa zaidi ya watu milioni tano wanaugua malaria.
Uchumi katika nchi hizi unaathiriwa sana na watu wanakuwa maskini kwa sababu ya vifo kuongezeka, na wanaougua malaria wanakuwa na uwezo mdogo wa kujihusisha na shughuli za kilimo.
Dawa zinazonunuliwa kutoka nchi za nje huwa ni ghali sana, na upatikanaji wake huwa ni mgumu katika nchi nyingi. Hali hii imesababisha kuwepo na ugumu .., na ukosefu wa fedha kwa ajili ya upatikanaji wa ACT. Continue reading