Malaria – maono na uzoefu wa anamed

Translated by Frank Jacob

Utangulizi
Katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara malaria inaua kati ya watu milioni moja hadi mbili kila mwaka, haswa watoto. Utafiti wa karibuni (Machi 2005) umeonyesha kuwa zaidi ya watu milioni tano wanaugua malaria.
Uchumi katika nchi hizi unaathiriwa sana na watu wanakuwa maskini kwa sababu ya vifo kuongezeka, na wanaougua malaria wanakuwa na uwezo mdogo wa kujihusisha na shughuli za kilimo.
Dawa zinazonunuliwa kutoka nchi za nje huwa ni ghali sana, na upatikanaji wake huwa ni mgumu katika nchi nyingi. Hali hii imesababisha kuwepo na ugumu .., na ukosefu wa fedha kwa ajili ya upatikanaji wa ACT.

Majibu ya kawaida ni hakuna ufumbuzi
1. Kuna kampeni ya kimataifa ya kufanya dawa zinazozalishwa na kampuni za dawa katika nchi za magharibi kuwa nafuu, ili watu wengi ambao ni wagonjwa waweze kulipia dawa hizo. Lakini hata upunguzaji wa asilimia tisini (90%) bado hautasaidia jamii kubwa ambao wengi wao wanaishi vijijini.
2. Nchi zilizo nyingi hupulizia DDT. Hii ni kemikali ya sumu, mojawapo ya kemikali za uchafuzi wa mazingira. Huwa haiishi kwa muda wa mika mingi, haiui mbu tu bali hata wadudu na ndege wenye manufaa, hivyo kufikiriwa kuongeza kwa kiwango cha saratani.
3. Nchi nyingi zinatengeneza na kuhakikisha vyandarua kwa wajawazito vinapatikana katika bei nafuu. Hata hivyo hii sio desturi kwa watu wengi kutumia vyandarua au kuweka nyavu kwenye madirisha.
4. Shirika la Afya Duniani linafahamu juu ya umuhimu wa Artemisia annua, na viwanda vya kuzalisha madawa vimezalisha kwa wingi artemisinin kwa ajili ya dawa kama vile Artesunate, Artemax na Riamet. Katika baadhi ya nchi dawa hizi zimekuwa ndio chaguo la kwanza kwa ajili ya matibabu. Lakini mwaka 2005, kumetokea uhaba mkubwa wa majani makavu ya Artemisia.
5. Utafiti bado unaendelea ili kutafuta chanjo ya malaria. Ingawa kuna mafanikio yameonekana, bado upatikanaji wa chanjo umekuwa mgumu.
6. Baadhi ya waganga wamegundua jinsi ya kutibu malaria. Lakini, mara nyingi wamekuwa wakifanya ni siri, na kutotoa maelezo kamili ya dozi, wanaziandaa katika hali isiyokuwa na usafi na mara zote wanaziuza kwa bei ya juu.

Mfumo wa hatua kwa dawa za asili
“Anamed” ni ufupisho wa hatua kwa dawa za asili”, ni mtandao wa kimataifa wa maendeleo kwa wafanyakazi, madaktari,wauguzi na waponyaji kwa kubadilishana maarifa kimatibabu na uzoefu katika nchi za kitropiki.
Anamed maana yake ni muungano wa faida za madawa ya jadi (mfano kutumia miti shamba ) na zile za huduma za tiba za kisasa zenye msingi wa kisayansi (mfano usafi, umezaji wa vidonge kiumakini) semina za Anamed inaruhusu aina nyingi ya mimea ambayo imekubaliwa kutumiwa kwa matibabu ya Malaria.mfano papai, kahawa, mwarobaini, na mwingajini.

Artemisia - Frank Jacob in Matanana

Artemisia – Frank Jacob, Matanana/Tanzania

Mmea mwingine ambao umetumiwa China kwa muda wa miaka elfu mbili(2000) kwa kutibu malaria ni Artimisia annua kwa uweza wa kuzuia malaria umejulikana miaka ishirini na tano(25) iliyopita. Artimisia haipatikani au haistawi katika nchi za kitropiki.
Anamed imeanza kilimo cha Artimisia kwa hali ya juu kwa kupanda mashamba zaidi yamia sita (600) katika zaidi ya nchi sabini (70).Tukiongezea Anamed ni kampuni ya kwanza Duniani kuchapisha matokeo ya matibabu kwa wagonjwa baada ya kunywa chai ya Artimisia. Hii tunaiita Artimisia annua anamed.
Artimisia annua Anamed haijatengenezwa tu na artimisia pekee bali baadhi ya dawa za asili ambazo zinatibu malaria. Mmea huu huvunwa zaidi ukanda joto na chai iliyotengenezwa kwa majani ya artimisia inaonesha kwamba inatibu malaria.
Jinsi anamed itakavyotekelezwa
1. Kila hospitali na kituo cha afya katika nchi yoyote itaandaa eneo la bustani kwa ajili ya kuotesha artimisia zimeazisha bustani ya artimisia na dawa nyingine za asili za kuzuia malaria, Pia maduka ya dawa yaliyo katika hospitali hizo watavuna majani na kuyakausha na kufunga katika pakiti ili wauguzi waweze kutoa dawa hizo kama chai.
Kwa njia hiyo kila hospitali itaweza kujitegemea kifedha kutibu malaria, Ingawa kutakuwa na wagonjwa ambao itabidi wapewe dawa za kisasa.
2. Zahanati, vituo vya afya na wataalamu wa dawa asilia pia wataotesha dawa hiyo hivvyo kuweza kutoa tiba kama wataalamu wengine wa hospitali watakavyofanya.

Ni jinsi gani Anamed inatumika
1. Kupitia uwazi wa serikali inavyojitolea katika mchakato huu.
2. Kufundisha uvunaji, kuandaa chai ya artimisia na matibabu ya wagonjwa hospitarini, madaktari, wauguzi, maduka ya madawa na waganga wa asili
3. Kupitia msaada wa taasisi za utafiti nchini.
Uzoefu wa Anamed ni pale maandiko yanapotekelezwa kwa vitendo.
1. Ndogo lakini inapendeza, kila kliniki inauhuru wa kutibu malaria, Nafasi muhimu za kazi zinapatikana kila sehemu, kila sehemu inaweza kufanya maendeleo ya matibabu ya malaria kwa maeneo yanayohusika, gharama za kutibu malaria zinakuwa zimepungua.
2. Kuna uhakika wa kupatikana kwa dawa za kutosha za asili za malaria. Hakuna matatizo ya fedha za kigeni na mipaka katika kuzisambaza nchini.
3. Watu binafsi na familia zao kwa wakati wanaelewa matibabu na wanaweza kujitibu wenyewe. Vilevile hali hizo inawafanya watu wengi kupata maendeleo na kuchukua majukumu kwa afya zao hivyo kupunguza msongamano sehemu za zahanati, hali inayotoa nafasi kwa zahanati kutibu magonjwa mengine sugu.
4. Kutokuaminiana kati ya wataalamu wa dawa za asili na dawa za hospitalini kunasababisha kuwepo kwa njia ya ushirikiano katika ujuzi na uzoefu wa kuchangia na kujadili

ANAMED